Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia zazinduliwa Nairobi

Kaulimbiu ya mwaka huu ni, “Ungana Kukomesha Ukatili dhidi ya Wanawake na Wasichana: Hakikisha Haki Inatendeka, Linda Waathiriwa na Komesha Kutoadhibiwa kwa Wahalifu.”

Marion Bosire
1 Min Read

Serikali ya Kaunti ya Nairobi, kwa ushirikiano na Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma, ODPP, na wadau wengine, imezindua rasmi kampeni ya mwaka 2026 ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia.

Usimamizi huo wa gatuzi la jiji kuu la Kenya, imetoa wito wa kuimarishwa kwa juhudi za kulinda wanawake na wasichana.

Kampeni hiyo ilizinduliwa Jumatano, Novemba 25, 2026, katika Shule ya Upili ya Eastleigh na kuhudhuriwa na mashirika ya serikali, mashirika ya kijamii, wanafunzi na wawakilishi wa jamii.

Kampeni hiyo ya kimataifa inaanza Novemba 25 hadi Desemba 10, ikiwa na kaulimbiu: “Ungana Kukomesha Ukatili dhidi ya Wanawake na Wasichana: Hakikisha Haki Inatendeka, Linda Waathiriwa na Komesha Kutoadhibiwa kwa Wahalifu.”

Kupitia kampeni hiyo, Kaunti ya Nairobi inapanga kuendesha mijadala ya uhamasishaji katika kaunti zote ndogo 17 ili kukabiliana na visababishi vya ukatili wa kijinsia.

ODPP imesisitiza dhamira yake ya kuhakikisha kesi za ukatili wa kijinsia zinaendeshwa ipasavyo mahakamani na waathiriwa wanapata haki.

Vilevile, viongozi wa kaunti wamehimiza kuimarishwa kwa huduma za afya, usaidizi wa kisaikolojia na msaada wa kisheria kwa waathiriwa.

Share This Article