Baraza la Mawaziri nchini Israel limeidhinisha na kutangaza kufungwa kwa shule zote kwa siku mbili huku vita vya majeshi yake dhidi ya wanamgambo wa Kipalestina, Hamas vikiingia siku ya pili.
Wapalestina zaidi ya 300 wameuawa kwenye mashambulizi yanayotekelezwa na majeshi ya Israel katika ukanda wa Gaza.
Israel imetangaza kuwa zaidi ya raia wake 600 wameuawa.
Kundi la Hezbollah limetangaza leo Jumapili kuwa limetekeleza mashambulizi katika eneo la mashamba ya Shebaa na kuwaua raia kadhaa wa Isreal kama njia ya kuunga mkono Palestina.
Viongozi mbalimbali ulimwenguni wamelaani vita hivyo ambavyo huenda vikasababisha maafa zaidi.