Shule kadhaa zawarejesha wanafunzi nyumbani

Dismas Otuke
1 Min Read

Shule kadhaa katika mitaa ya kaunti ya Nairobi zimewarejesha wanafunzi nyumbani licha ya agizo la serikali la jana Jumatano kuzitaka shule zote za kutwa kaunti za Nairobi, Mombasa na Kisumu kufunguliwa leo.

Shula kadhaa za mitaa ya Kibra na Kangemi ziliripotiwa kuwataka wanafunzi waliofika shuleni kwa masomo kurejea nyumbani kwa kuhofia usalama wao.

Baadhi ya shule ziliwataka wanafunzi kurejea shuleni kesho Ijumaa, yamkini lengo likiwa kutathmini hali ya usalama zenyewe hata baada ya serikali kuwataka wanafunzi kurejea shuleni.

Maandamano ya upinzani dhidi ya serikali yaliyoanza jana Jumatano yanaingia siku ya pili leo Alhamisi.

Kangemi na Kibra ni baadhi ya mitaa kaunti ya Nairobi, ambayo imekumbwa na visa vingi vya maandamano na uharibifu wa mali.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *