Timu ya taifa ya raga ya Kenya kwa wachezaji saba kila upande ilikosa kufuzu kwa mashindano ya msururu wa Dunia msimu ujao baada ya kumaliza ya tisa katika mashindano ya kufuzu yaliyokamilika Jumapili.
Kenya ilimaliza ya tisa baada ya kumaliza ya 11 katika msururu wa tatu na wa mwisho wa Bordeaux uliokamilika Jumapili jioni na kuzoa alama 2.
Marekani iliyochukua nafasi ya tano katika msururu huo wa mwisho iliipiku Kenya na kumaliza ya nane kwa jumla ya pointi 17, kutokana na misururu mitatu, alama 1 zaidi ya Kenya.
Kenya ilifuzu kwa robo fainali ya kombe kuu katika misururu miwili ya Hong Kong na Valladolid.
Afrika Kusini ilitwaa ubingwa kwa alama 52, ikifuatwa na New Zealand kwa pointi 44,2 zaidi ya Uhispania iliyotwaa nafasi ya tatu.
Timu zingine zilizofuzu kwa mashindano ya dunia msimu ujao ni Australia, Argentina, Fiji, Ufaransa na Marekani zilizochukua nafasi za 4, 5, 6, 7 na 8 mtawalia.