Mchekeshaji Eric Omondi aachiliwa huru kwa dhamana ya laki moja

Omondi alishinda korokoroni wikendi iliyopita baada ya kukamatwa kwake.

Dismas Otuke
1 Min Read

Mchekeshaji Eric Omondi leo Jumatatu adhuhuri aliachiliwa huru kwa dhamana ya shilingi laki moja na Mahakama ya Milimani.

Omondi anakabiliwa na kesi ya kuleta msongamano wa magari kwenye barabara ya Kimathi mwezi jana.

Alishinda korokoroni wikendi iliyopita baada ya kukamatwa kwake.

Mchekeshaji huyo anaaminika kusababisha msongamano wa magari tarehe 18 mwezi jana kwenye barabara ya Kimatahi aliporusha mitungi ya maji.

Wakili wa Omondi, Danstan Omari, amesema kamwe mitungi hiyo iliyokuwa imejaa lori haikulenga kusababisha msongamano bali ilikuwa ikipelekewa watu walio na uhaba wa maji katika kaunti ya Nairobi.

Share This Article