Shujaa yalenga robo fainali Hong Kong Sevens

Dismas Otuke
1 Min Read

Timu ya taifa ya Kenya ya raga kwa wachezaji saba upande maarufu kama Shujaa inalenga kucheza hadi robo fainali katika mkondo wa mashindano ya Hong Kong  Sevens, utakaoandaliwa kati ya tarehe 17 na 19 mwezi huu.

Nahodha wa timu hiyo Samuel Asati amesema wanalenga ushindi katika mechi ya ufunguzi dhidi Australia .

“Tumejiandaa vyema lengo letu tuu ni kuwa miongoni mwa timu anne ziatakazofuzu kwa mashindano ya dunia msimu ujao,tunalenga kufika robo fainali Hong Kong na tunataka kumaliza katika nafasi nane za kwanza baada ya misururu mitatu ijayo.”akasema Asati

Upande kocha mkuu Kevin Wambua aliwapongeza mashabiki wote kwa kuiunga mkono timu katika mechi za divisheni ya pili.

“Tumeamua kama timu lazima tuweke mchezo wetu wa hali ya juu na nina imani tutaanza vyema dhidi ya Australia tukiangazia kuwa miongoni mwa timu nane bora mwisho wa msimu.”akasema Wambua

Kenya imejumuishwa kundi C katika msururu wa wikendi ijayo pamoja na  Newzealand,Australia na Marekani.

 

 

 

Share This Article