Wanariadha wa Kenya wawasili Guangzhou kwa mbio za dunia za kupokezana kijiti

Kenya inashiriki mashindano hayo ikilenga kutimiza muda wa kufuzu kwa mashindano ya dunia ya mwezi Septemba mjini Tokyo,Japan.

Dismas Otuke
1 Min Read

Timu ya Kenya kwa mbio za Dunia za kupokezana kijiti imewasili mjini Guanghou,Uchina leo tayari kwa mashindano hayo yatakayoandaliwa Jumamosi na Jumapili hii Mei 10 na 11.

Kikosi hicho cha wanariadha takriban 20 kiliondoka jana jioni.

Kenya inashiriki mashindano hayo ikilenga kutimiza muda wa kufuzu kwa mashindano ya dunia ya mwezi Septemba mjini Tokyo,Japan.

Timu hiyo itaongozwa na bingwa wa Jumuiya ya Madola katika mbio za mita 100 Ferdinand Omanyala, atakayeshiriki mbio za mita 100 kwa wanariadha wanne huku Boniface Mweresa akiwa nahodha.

Kenya itashiriki kati faini za mita 400 kwa wanariadha wanne kupokezana kijiti kwa wanaume na wanawake na ile ya mseto,mbio za mita 100 kwa wanariadha wanne kupokezana kijiti wanaume.

 

 

 

Website |  + posts
Share This Article