Shujaa wateleza dhidi ya Marekani, mashindano ya HSBC

Dismas Otuke
1 Min Read

Timu ya raga ya Kenya kwa wanaume saba, upande maarufu kama Shujaa, imeanza vibaya divisheni ya pili ya mashindano ya msururu wa pili wa dunia huko Uruguay, baada ya kulemewa alama 10-14 na Marekani Jumamosi jioni.

John Okeyo and Vincent Onyala walifunga try za Kenya kunako dakika za 1 na 4, kabla ya Marekani kusawazisha kupitia kwa David dakika ya 5 na Orrin Bizer dakika tatu baadaye na  wakaunganisha  conversions.

Kenya itarejea uwanjani kwa mchuano wa pili mapema kesho dhidi ya Ubelgiji.

Shujaa ilimaliza ya tatu kwa pointi 16 kwenye msururu wa kwanza ulioandaliwa mwezi jana katika uwanja wa Nyayo.

 

Share This Article