Shujaa warushwa kundi gumu michezo ya Olimpiki

Dismas Otuke
1 Min Read

Timu ya taifa ya raga ya Kenya kwa wacehzaji saba upande ya wanaume,Shujaa imejumuishwa kundi gumu katika michezo ya Olimpiki ya mwaka huu jijini Paris Ufaransa itakayoanza mwezi mmoja ujao.

Kenya imerushwa kundi B pamoja na mabingwa mara saba  Argentina, Australia na  Samoa.

Shujaa itakuwa ikishiriki michezo ya Olimpiki kwa mara ya tatu mtawalia na watalenga kufuzu kwa hatua ya mwondoano, baada ya kubanduliwa katika hatua ya makundi mwaka 2012 na 2020.

Mabingwa watetezi New Zealand wamo kundi A pamoja na Ireland,Afrika Kusini na Japan, wakati kundi C likisheheni Fiji, wenyeji Ufaransa ,Marekani na Uruguay.

Raga ya wanaume itaandaliwa kati ya Julai 24 hadi 27 .

Website |  + posts
Share This Article