Timu ya taifa ya raga ya Kenya kwa wachezaji saba kila upande, Shujaa, ilizoa pointi tatu kwenye msuru wa tatu wa raga duniani uliokamilika jana mjini Perth, Australia.
Shujaa ilimaliza ya 10 kwenye msururu huo baada ya kulemewa na New Zealand alama 19-12 katika mechi ya kuwania nafasi ya tisa.
Shujaa inayoongozwa na Kevin Wambua, ilikuwa imesajili ushindi mmoja pekee alama 19-15 dhidi ya Uriguay katika kundi C, baada ya kushindwa na Newzealand na Fiji.
Katika nusu fainali ya kuwania nafasi ya tisa, Kenya iliibwaga Marekani alama 26-21.
Kenya ni ya 9 katika msimamo wa dunia kwa alama 14, na sasa wanaangazia msururu wa nne wa Vancouver, Canada, kati ya tarehe 21 na 23 mwezi ujao.
Fiji, Argentina, na Uhispania zinaongoza msimamo kwa pointi 48 kila moja baada ya mikondo mitatu ya ufunguzi wa msimu.