Timu za Kenya Shujaa na Kenya Lionesses zilitwaa ubingwa wa makala ya mwaka huu ya mashindano ya raga kwa wachezaji saba upande ya Safari Sevens yaliyokamilika Jumapili jioni katika uwanja wa kitaifa wa Nyayo.
Shujaa ilinyakua taji ya wanaume kwa mara ya tano mtawalia kufuatia ushindi wa alama 24-5 dhidi ya Morans .
Timu ya wanawake ya Lionesses ilinyakua taji baada ya kuwashinda Uganda pointi 22-5 kwenye fainali.
Mashindano hayo ya siku tatu yalishirikisha timu 12 za wanaume na wanawake.