Timu ya taifa ya raga ya Kenya kwa wachezaji saba upande – Shujaa, itashiriki mashindano ya divisheni ya kwanza, baada ya kushushwa ngazi kutoka msururu wa dunia.
Hii ni baada ya waandalizi wa mashindano ya HSBC Sevens kutangaza kuwa timu za msururu huo zitasalia 8 kuanzia msimu ujao na wala sio 12.
Uamuzi huo una maana kuwa timu sita bora kutoka mashindano ya mchujo ya Los Angeles, Marekani, baina ya leo na kesho, zitashiriki mashindano ya divisheni ya kwanza.
Hii ina maana kuwa Shujaa Pamoja na Kenya Lionesses ni sharti wamalize miongoni mwa nafasi nne za kwanza, ili kufuzu kwa mashindano ya Division One msimu ujao.
Kwa jumla, kutakuwa na vitengo vitatu vya mashindano ya raga duniani kuanzia mwaka ujao;mashindano ya msururu yatakayoshirikisha mataifa manane na mashindano ya Division 1 yatakayokuwa na timu 8 huku timu sita zikishiriki yale ya Division 2.
Shujaa ilimaliza ya tisa katika msururu wa dunia wa mwaka 2024 na 2025.