Timu ya taifa ya raga ya Kenya kwa wachezaji saba kila upande itachuana na Ireland leo usiku. Mechi hiyo itakuwa ya kuwania nafasi ya 11 na 12 katika msururu wa nne wa mashindano ya dunia ya Vancouver nchini Canada.
Kenya imepoteza mechi zote nne ilizocheza huko Vancouver.
Shujaa ilishindwa mechi tatu za kundi A dhidi ya Uingereza, Ufaransa na Argentina, kabla ya kulemewa na Uruguay katika mechi ya kuwania nafasi za 9 na 10.