Shirika la Msalaba Mwekundu, limetia saini mkataba wa maelewano na serikali ya kaunti ya Busia, kuimarisha uwezo wa kaunti hiyo katika kukabiliana na majanga.
Maswala makuu katika mkataba huo ni mafunzo kuhusu kujitayarisha kwa majanga, ambapo shirika la Msalaba Mwekundu litafadhili utoaji mafunzo hayo kwa maafisa wa kaunti ya Busia.
Mkataba huo pia unajumuisha ushirikiano wa kushughulikia dharura, utakaolainisha ushirikiano baina ya shirika hilo na serikali hiyo ya Busia wakati majanga yanapozuka.
Aidha mkataba huo unaangazia mipango ya kuhamasisha umma, kuwaelimisha kuhusu hatari za majanga na mikakagi ya kujiandaa kushughulikia majanga hayo.
Ushirikiano huo unalenga kuboresha uwezo wa kaunti hiyo kukabiliana na majanga na hivyo kuokoa maisha ya wakazi wa kaunti hiyo.