Shirika la Kenya Airways lapata faida ya shilingi milioni 513

Tom Mathinji
1 Min Read
Ndege ya shirika la Kenya Airways.

Baada ya kunakili hasara kwa muda wa miaka kumi iliyopita, sasa shirika la ndege la Kenya Airways, KQ lina kila sababu ya kutabasamu baada ya kupata faida ya shilingi milioni 513 katika nusu ya kwanza ya mwaka huu.

Katika kipindi kilichokamilika Juni 30,2024, mapato ya  KQ yaliimarika kwa asilimia 22 kutoka shilingi bilioni 75.1 hadi shilingi 91, hali iliyotajwa kuchochewa na idadi kubwa ya wasafiri katika kipindi hicho.

Afisa Mkuu wa masuala ya fedha wa KQ Hellen Mwariri alisema faida hiyo iliimarika kwa asilimia 102 baada ya kupata hasara ya shilingi bilioni 21.7 ambayo shirika hilo lilipata katika kipindi kama hicho mwaka uliopita.

Mwenyekiti wa shirika hilo Michael Joseph, alisema ufanisi huo umetokana na juhudi kamambe zilizotekelezwa na wanachama wa bodi ya wasimamizi, viongozi na wafanyakazi wa shirika hilo.

Kwa upande wake, Mwariri alisema faida hiyo iliimarika kwa asilimia 102 baada ya kupata hasara ya shilingi bilioni 21.7 ambayo shirika hilo lilipata katika kipindi kama hicho mwaka uliopita.

Mwariri aliongeza kuwa jumla ya gharama za utoaji huduma  zilipungua kwa asilimia 22 hadi shilingi bilioni 90.20 na hivyo kuchangia ongezeko la faida kwa asilimia 30 hadi shillingi billioni 1.30.

Website |  + posts
Share This Article