Mwanahabari wa runinga ya KBC Shiksha Arora ametangaza kuondoka katika kituo hicho baada ya kukifanyia kazi kwa miaka mitatu.
Kwenye ujumbe aliouchapisha kwenye mtandao wa kijamii, alielezea skukrani na hisia mseto kuhusu kuondoka kwake.
‘’Moyo wangu umejaa hisia ninapo andika haya. Ni vigumu kusema kwaheri sehemu ya kazi ambayo nimeita nyumbani kwa miaka mitatu na wenzangu ambao wamekuwa kama familia’’ aliandika.
Alishukuru watazamaji na wafanyakazi wenza kwa kujiunga naye katika safari hiyo.
“Tumecheka, tukacheza, tukalia na kustawi pamoja”.
Kabla ya kujiunga na KBC, alifanya kazi katika runinga na redio moja ya humu nchini. Akiwa nchini Uingereza, alihudumia kituo cha BBC na Smoke FM.
Katika masomo, anamiliki shahada ya sayansi katika matibabu ya Biolojia na Bioteknolojia.
Anapoondoka, gwiji huyo wa habari za saa tatu Ijumaa ameashiria ukurasa mpya wa siku za halafu.
“Huu sio mwisho wa maonyesho ila mwanzo wa ukurasa ambao ninafurahia’’.
Shiksha atawaaga mashabiki na watazamaji wa KBC kwa ujumla rasmi hii leo Ijumaa kwenye habari zake za mwisho.