Serikali imezindua mpango wa kuwashirikisha wakimbizi katika jamii kwa jina Shirika Plan, ambao utahakikisha wanatangamana vyema na jamii na kuishi katika mazingira bora.
Akizungumza wakati uzinduzi wa mpango wa Shirika Plan, katika Ikulu ya Nairobi, Rais William Ruto alielezea umuhimu wa kuwajumuisha wakimbizi katika ukuaji wa maendeleo nchini.
“Mpango huo utawiainisha mazingira wanayoishi wakimbizi na kutambua mchango wao muhimu katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi humu nchini,” alisema Rais Ruto.
Aidha kiongozi wa taifa alisema mpango huo utashughulikia kikamilifu maswala ambayo wakimbizi wameibua.
Balozi wa Umoja wa Mataifa anayehusika na maswala ya wakimbizi Filipo Grandi aliyehudhuria hafla hiyo, alielezea jukumu muhimu linalotekelezwa naKenya katika kuwahifdhi wakimbizi .
Wengine waliohudhuria hafla hiyo ni pamoja na Naibu Rais Prof. Kithure Kindiki, Gavana wa Turkana Jeremiah Lomorukai na mwenzake wa Garissa Nathif Jama.