Wabunge wana kila sababu ya kutabasamu baada ya serikali kutoa shilingi bilioni 6 za kustawisha maeneo bunge nchini, NG-CDF.
Hii inafuatia shinikizo kutoka kwa wabunge wa mirengo ya Kenya Kwanza na Azimio waliotishia kumtimua afisini Waziri wa Fedha Njuguna Ndung’u, kwa kuchelewesha kutoa pesa hizo.
Kila eneo bunge limepokea mgao wa shilingi milioni 20, kikiwa ni kiwango cha kwanza cha fedha zilizotolewa na serikali kufadhili maeneo bunge katika kipindi cha bajeti cha mwaka 2023 na 2024.
Hata hivyo, kiwango hicho kina upungufu wa shilingi bilioni 4 kutoka shilingi bilioni 10 zilizoahidiwa na Rais William Ruto.