Serikali yatoa shilingi bilioni 3.5 za mpango wa Inua Jamii za mwezi Disemba

Fedha hizo zilianza kusambazwa kwa wanufaikaji Jumanne, Januari 7, 2025. Majaribio ya kuwalipa wanufaikaji kwa njia ya MPesa kuanzia mwezi huu kwa sasa yanafanyika katika kaunti za Murang'a na Marsabit.

Martin Mwanje
1 Min Read
Joseph Motari - Katibu katika Wizara ya Leba

Serikali imetoa shilingi bilioni 3.517,470,000  zitakazogawiwa watu milioni 1,758,735 waliojiandikisha kwenye mpango wa Inua Jamii. 

Fedha hizo zilizotolewa na Wizara ya Leba kupitia Idara ya Utunzaji wa Jamii na Masuala ya Wazee ni za mwezi Disemba mwaka jana.

Katibu wa Idara hiyo Joseph Motari anasema malipo yalianza kutolewa jana Jumanne huku kila mnufaikaji akitarajiwa kupokea shilingi 2,000 za kipindi cha mwezi Disemba.

Ili kurahisisha usambazaji wa fedha hizo wa wanufaikaji, Motari anasema serikali inafanya majaribio ya kuwalipa wanafukaji kwa nia ya MPesa.

“Ili kuboresha utoaji huduma, idara inafanya majaribio ya mfumo mpya wa malipo kwa kutumia MPesa kupitia mfumo wa e-Ciizen,” amesema Katibu huyo kwenye taarifa.

“Kuanzia mwezi Januari, 2025, wanaufaikaji wote chini ya mpango huo watalipwa kupitia mfumo mpya.”

Majaribio hayo kwa sasa yanafanyika katika kaunti za Murang’a na Marsabit huku wanufaikaji katika kaunti zingine zote wakipokea malipo kupitia akaunti zao za kawaida za benki.

Mpango wa Inua Jamii huwalenga watu wanaoishi katika mazingira magumu kama vile wazee, mayatima na watu wanaoishi na ulemavu wa kiwango cha juu.

Lengo la mpango huo ni kuwsaidia wote hao kujikimu kimaisha.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *