Serikali ya Kenya kupitia Idara ya Jinsia na tende sawazishi , imetoa shilingi bilioni 1.5 kusaidia makundi mbalimbali ya utekelezaji miradi ya kijamii katika kaunti zote 47 nchini.
Fedha hizo zitagharamia karo za shule kwa wanafunzi kutoka familia zisizojiweza kulingana na sheria ya serikali ya kitaifa kuhusu hazina ya kitaifa ya tende zawazishi (NGAAF).
Shilingi milioni 273 zimetolewa kama msaada wa masomo kwa wanafunzi 25,000, ili kuwawezesha kupata fursa za elimu na ujuzi .
Hazina hiyo pia imetoa shilingi milioni 413 kusaidia makundi 2,000 yaliyosajiliwa kupata ruzuku kwa za kujiendeleleza kijamii na kiuchumi na miradi ya ya kuongeza tija.
Zaidi ya hayo, shilingi milioni 677 zimetolewa kwa miradi ya kaunti ambayo manufaa yake yatapatikana katika sehemu mbalimbali katika kaunti 47 nchini.
Ili kuhakikisha mtagusano wa jamii , hazina hiyo imetoa shilingi milioni 137 kuwaelimisha wananchi kupitia uhamasishaji wa umma, kuhusu mipango na sera mbalimbali za serikali na jinsi ya kupata fedha za NGAAF na fedha nyingine zilizogatuliwa.
Mbinu za kutoa elimu kwa umma zinalenga kuhakikisha kuongezeka matumizi ya programu za serikali.
Watakaonufaika kwa ruzuku hizo ni makundi ya kujisaidia ambayo yalituma maombi na kuafiki vigezo vilivyowekwa kupitia kwa ofisi za za NGAAF, katika kaunti 47 kufikia tarehe 3 Aprili 2024.