Serikali yatangaza kesho Ijumaa kuwa sikukuu ya Idd

Sikukuu ya Idd husherehekewa na Waislamu wote kote duniani kuashiria kukamilika kwa siku 30 za mfungo wa Ramadhani.

Dismas Otuke
1 Min Read

Wizara ya Usalama wa Taifa imetangaza kesho Ijumaa, Machi 20, kuwa sikukuu ya Idd Ul Fitr.

Waziri wa Usalama wa Taifa Kipchumba Murkomen alichapisha kwenye gazeti rasmi la serikali kuwa Ijumaa tarehe 20 mwezi huu itakuwa sikukuu.

Sikukuu ya Idd husherehekewa na Waislamu wote kote duniani kuashiria kukamilika kwa siku 30 za mfungo wa Ramadhani.

Mfungo wa Ramadhani huwa ni mwezi mtakatifu kwa Waislamu ambao hufunga kula na kunywa kutoka macheo hadi machweo wakipiga dua.

Ramadhani ni mojawapo wa nguzo kuu tano za dini ya Uislamu, na sherehe za Idd huadhimisha kukamilika kwa mfungo huku ndugu, jamaa na marifiki wakiandaa sherehe na pia kuwakumbuka wasiobahatika katika jamii wakati wa Idd kwa kula pamoja au kutoa msaada wa vyakula.

Share This Article