Wizara ya usalama wa ndani imetangaza kesho Ijumaa, Machi 20, kuwa siku kuu ya Idd Ul Fitr.
Waziri wa usalama wa ndani Kipchumba Murkomen alichapisha kwenye gazeti rasmi la serikali kuwa Ijumaa tarehe 20 mwezi huu itakuwa siku ya mapumziko.
Siku kuu ya Idd husherehekewa na Waislamu wote kote duniani kuashiria kukamilika kwa siku 30 za mfungo wa Ramadhan.
Mfungo wa Ramadhan huwa ni mwezi mtakatifu kwa Waislamu ambao hufunga kula na kunywa kutoka macheo hadi machweo wakipiga dua.
Ramadan ni mojawapo wa nguzo kuu tano za dini ya Uislamu, na sherehe za Idd huadhimisha kukamilika kwa mfungo huku ndugu, jamaa na marifiki wakiandaa sherehe na pia kuwakumbuka wasiobahatika katika jamii wakati wa Idd kwa kula pamoja au kutoa msaada wa vyakula.