Serikali yapiga marufuku uvunaji Macadamia hadi Machi 2025

Tom Mathinji
1 Min Read
Waziri wa kilimo Dkt. Andrew Karanja.

Wizara ya kilimo imepiga marufuku uvunaji wa Macadamia kuanzia Novemba 2, 2024 hadi Machi 1, 2025.

Kulingana na wizara hiyo, hatua hiyo inalenga kukabiliana na uuzaji wa Macadamia ambayo hayajakomaa.

Waziri wa kilimo Andrew Karanja, alisema uamuzi huo uliafikiwa baada ya mashauriano na wadau katika sekta hiyo, akidokeza kuwa shirika la kilimo na chakula AFA, limejukumiwa kutekeleza agizo hilo.

“Halmashauri hiyo itazidisha uchunguzi wake kuwafurusha wanabiashara walaghai,” alisema waziri Karanja.

Dkt. Karanja alielezea kuwa alisema soko kubwa la Macadamia ni nchi za kigeni, ambapo Kenya huuza asilimia 95 za zao hilo katika soko la nje.

Aidha Dkt. Karanja alisema hatua hiyo pia itasaidia kuimarisha bei ya Macadamia.

Ili kufanikisha agizo hilo, waziri huyo alisema wakulima watalazimika kuwasilisha kiwango cha Macadamia walicho nazo kwa ukaguzi kufikia Novemba 15,2024.

TAGGED:
Share This Article