Serikali imeondolea mbali marufuku ya wafugwa kutemebelewa gerezani, ambayo yamedumu miaka minne, ili kutoa fursa kwa wafungwa kuunganishwa tena na jamaa zao.
Huku akiondolea mbali mafurukufu hayo, waziri wa usalama wa taifa Prof. Kithure Kindiki, alisema kuanzia mwezi ujao wa Machi, wafungwa wataanza kutembelewa gerezani na familia zao mara moja baada ya kila miezi sita.
Mpango huo wa kuwatembelea wafungwa ulisitishwa mwaka 2020 kutokana na janga la COVID-19.
Alipozuru gereza la Naivasha siku ya Jumatano, waziri Kindiki alisema kutokana na kuisha kwa janga la Covid-19, sasa wafungwa wana fursa ya kuunganishwa na familia zao.
“Tumeondoa marufuku ya wafungwa kutembelewa, na kuanzia sasa familia zina fursa ya kuwatembelea wafungwa,” alisema waziri Kindiki.
Marufuku hayo ya kuwatembelea wafungwa, awali yalinuia kudumu kwa siku 30 lakini muda huo ulirefushwa na haujawai kuondolewa hadi siku ya Jumatano.