Serikali yafutilia mbali madeni yanayodaiwa wakulima wa kahawa

PCS
By
PCS
1 Min Read
Rais William Ruto aongoza mkutano wa baraza la mawaziri.

Baraza la mawaziri limeidhinisha kufutiliwa mbali kwa madeni yanayodaiwa wakulima wa kahawa na marekebisho mengine yanayopasa kufanyiwa sekta ya kahawa.

Wakati wa mkutano wa baraza la mawaziri ulioongozwa na Rais William ruto katika ikulu ya Nairobi Jumanne, baraza la mawaziri liliidhinisha kufutiliwa mbali madeni ya miaka mingi yanayodaiwa wakulima wa kahawa ya jumla ya shillingi billioni 6.8.

Baraza hilo la mawaziri lilisema, ili kuwezesha kulipwa kwa madeni hayo, vyama vya ushirika vya wakulima wa kahawa na taasisi zingine za kutoa mikopo zinapasa kuwasilisha kwa wizara ya ustawishaji wa vyama vya ushirika katika muda wa siku saba, orodha ya wakulima wanaodaiwa madeni na stakabadhi halisi ili zikaguliwe na kutayarisha malipo.

Kuhusu utekelezaji wa mpango wa afya kwa wote, baraza hilo liliidhinisha utaratibu wa mpito kutoka kwa hazina ya kitaifa ya bima ya matibabu hadi ile ya kitaifa ya afya kwa jamii kuanzia tarehe mosi mwezi Julai mwaka huu.

Ilipochukua hatamu za uongozi, serikali ya Rais William Ruto ilitoa ahadi ya kufanyia sekta ya kahawa mabadiliko ili kuiboresha zaidi, kuhakikisha wakulima wanafaidika na kilimo hicho.

PCS
+ posts
Share This Article