Serikali ya Kwale yatakiwa kuendelea kuboresha barabara

Kbc Digital
1 Min Read
Fatuma Achani - Gavana wa Kwale

Serikali ya kaunti ya Kwale imetakiwa kuendelea kuboresha miundombinu ya barabara ili kurahisisha usafirishaji wa bidhaa ndani na nje ya kaunti hiyo.

Wakazi wamepongeza juhudi za serikali ya kaunti hiyo za ujenzi wa barabara za lami na kutaka juhudi zaidi kufanywa ili kuboresha miundombinu katika kaunti hiyo.

Miongoni mwa barabara ambazo Gavana Fatuma Achani amefanikisha na kuendeleza uwekaji wa lami ni pamoja na barabara ya Tiwi-Magodzoni, Tsimba-Mbuguni, Kombani-Mferejini huko Matuga, Kona Polisi-Msambweni hospitali.

Barabara zingine ni Majoreni-Lungalunga  na Mkilo-Kalalani huko Kinango.

Wakazi hao wakiongozwa na Halima Mdoe wamesema kuwa ujenzi wa barabara za lami katika kaunti ya Kwale pamoja na uboreshaji wa miundombinu ya barabara imefungua uchumi wa kaunti hiyo ikilinganishwa na hapo awali.

Hadi kufikia sasa, serikali ya Kwale imejenga na kukarabati barabara za Kwale kwa takribani kilomita 3,833.

Serikali ya kaunti ya Kwale inalenga kukamilisha kilomita 6,833 za barabara ifikapo mwaka 2027.

TAGGED:
Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *