Afisa Mkuu wa kaunti ya Uasin Gishu anayesimamia Masuala ya Mifugo na Uvuvi Nixon Cheplong ametangaza mipango ya kuanzisha kiwanda cha kuchanganya malisho katika kaunti hiyo.
Amesema hatua hiyo inalenga kuwaondolea wafugaji wa kuku gharama kubwa za uzalishaji katika kaunti hiyo.
Cheplong aliyasema hayo wakati wa mkutano na wanachama wa Chama cha Biashara cha Sugoi kinachotoka wadi ya Tapsagoi, kaunti ndogo ya Turbo.
Wakati wa mkutano huo, afisa huyo aliwatia moyo wanachama hao akiwataka kutumia ipasavyo fursa zinazochipuka kuunga mkono shughuli zao za kilimo.
Chama cha Biashara cha Sugoi kwa sasa kinafuga zaidi ya vifaranga 4,000.