Serikali ya DRC kushiriki mazungumzo na M23 mwezi Aprili

Tom Mathinji
1 Min Read
Serikali ya DRC na waasi wa M23 kushiriki mazungumzo ya ana kwa ana mwezi Aprili.

Wapiganaji wa kundi la M23, wamesema kuwa watashiriki meza ya mazungumzo ya ana kwa ana kwa mara ya kwanza na serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, Aprili 9, 2025.

Kulingana na vyanzo vya habari nchini DRC, mkutano huo unatarajiwa kuandaliwa Jijini Doha, Qatar, huku yakiwa mazungumzo ya kwanza tangu M23 kuuteka mji wa Goma.

Hata hivyo, pande hizo mbili zimekubaliana kusalia kimya hadharani kuhusu mazungumzo hayo, huku yakikubaliana kutii masharti yaliyowekwa kuhusu mkutano huo.

Mapigano kati ya vikosi vya serikali ya DRC na waasi wa M23, yameyumbisha hali ya usalama Mashariki mwa nchi hiyo, huku  takriban watu 7,000 wakiuawa, wengi wakijeruhiwa na mamilioni wakitoroka makwao.

Hata hivyo, Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC, na ile ya Maendeleo Kusini mwa Afrika SADC, zimekuwa zikipanga mikakati ya kutafuta suluhu ya mzozo wa DCR.

Marais wa nchi wanachama wa Jumuiya hizo pamoja na wakuu wa vikosi vya usalama, wakiandaa mikutano ya mara kwa mara kwa lengo la kufanikisha upatikanaji wa amani nchini humo.

Jumuiya hizo kwa pamoja ziliwateua marais wa zamani kuwa wapatanishi kwenye mzozo huo, ambao ni Olusegun Obasanjo (Nigeria), Uhuru Kenyatta (Kenya), Sahle-Work Zewde (Ethiopia) na Catherine Samba-Panza wa Jamuhuri ya Afrika ya Kati.

TAGGED:
Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *