Serikali na Madaktari wakosa kuafikiana

Dismas Otuke
1 Min Read

Serikali na Madaktari wanaogoma walikosa kuafikiana Ijumaa usiku,  huku mgomo wa kitaifa ukiingia wiki ya nane katika hospitali zote za umma.

Kulingana na Waziri wa Afya Susan Nakhumicha, madaktari walikiuka agizo la mahakama kwa kukataa kusaini mwafaka huo na badala yake kuleta masharti mapya .

Kwa mjibu wa Mkuu  wa utumishi umma Felix Kosgei amesema walikosa kuafikiana baada ya madaktari kutaka kujumuishwa kwa matakwa mapya kinyume na agizo la mahakama.

Kikao cha Ijumaa kilitarajiwa kumaliza mgomo na madaktari wasaini mwafaka wa kurejea kazini.

TAGGED:
Share This Article