Serikali kushirikiana na vyuo vikuu kuimarisha sekta ya madini

Tom Mathinji
1 Min Read
Waziri wa madini na uchumi wa baharini Salim Mvurya.

Serikali imetangaza mipango ya kushirikiana na vyuo vikuu na wadau katika sekta ya uchimbaji madini, katika kufanya utafiti kuhusu thamani ya kiuchumi ya madini zilizopo hapa nchini.

Waziri wa madini, uchumi wa baharini na maswala  ya majini  Salim Mvurya, alisema wizara yake inashirikiana na vyuo vikuu kuimarisha utafiti na kutoa mafunzo kwa wahandisi na wataalm wa madini.

Akizungumza wakati wa kongamano katika kituo cha kenya na ujerumani kuhusu uchimbaji madini, mazingira, uhandisi na usimamizi wa rasilimali katika kaunti ya Mombasa, Mvurya alisema sekta ya uchimbaji madini ni muhimu sana hapa nchini, huku serikali ikikusudia kuongeza mapato kutoka asilimia moja ya pato jumla la taifa hadi asilimia 10 katika muda wa miaka mitatu.

Kulingana na waziri huyo, wizara yake inalenga kubuni sera za kusindika na kuongeza thamani, ambayo ni muhimu sana katika sekta hiyo inayoendelea kustawi.

“Tunataka kuboresha maabara, ili tutatue changamoto zinazotukumba za uchunguzi wa sampuli,”alisema  Mvurya.

“Ni muhimu sana kufanya kazi kwa pamoja na vyuo vikuu, ili wachangie katika mchakato huo,”aliongeza waziri huyo.

TAGGED:
Share This Article