Serikali inapania kupanua afisi ya idara ya uhamiaji kwenye kaunti ndogo ya Bungoma kusini, kwa lengo la kuwezesha idara ya uhamiaji kutayarisha na kutoa pasi za usafiri kwa wakazi wa sehemu hiyo.
Waziri wa usalama wa kitaifa Prof Kithure Kindiki alisema mipango inafanywa kukarabati afisi hiyo na kuongeza maafisa zaidi wa uhamiaji pamoja na vifaa vinavyohitajika.
Waziri alihuzunika kutokana na tatizo la kila mara la kucheleweshwa kwa utayarishaji na utoaji wa stakabadhi hizo muhimu za usafiri na akawahakikishia wakazi kwamba serikali inafanya kila juhudi kulainisha utaratibu wa utoaji wa pasi hizo za usafiri.
Kindiki aliyekuwa akiongea katika afisi ya kamishna wa kaunti ya Bungoma baada ya kuzuru afisi za idara ya uhamiaji huko Bungoma kusini na Lwakhakha, alisema marekebisho hayo yatatekelezwa kufikia mwezi june mwaka huu.
Kuhusu swala la usalama,waziri alisema mikakati muafaka imewekwa kuimarisha usalama kote nchini katika juhudi za kuhakikisha kwamba kila mkenya anaendelea na shughuli zake bila kuhofia wahalifu.