Serikali kujenga barabara ya Northern bypass kuwa ya safu mbili

Tom Mathinji
1 Min Read
Serikali kujenga barabara ya Northern bypass kuwa yenye safu mbili.

Katika juhudi za kuimarisha shughuli za uchukuzi na punguza msongamano, Baraza la Mawaziri Jumanne liliidhinisha pendekezo la kujenga barabara yenye safu mbili ya Northern bypass jijini Nairobi.

Barabara hiyo ya urefu wa kilomita 20.2, litafanikisha pakubwa shughuli za uchukuzi wa watu na bidhaa, na pia kudhibiti msongamano wa magari.

Mradi huo utaigeuza barabara hiyo ya safu moja kuwa ya pande mbili na kujumuisha ujenzi wa barabara za juu kwa juu na chini, na pia ujenzi wa mapito yasiyo ya magari, yakiwemo yale ya wanaotembea kwa miguu na baiskeli, kuimarisha mifumo ya uondoaji maji taka, na kuimarisha barabara zilizo karibu.

Barabara hiyo ambayo inaanzia Ruaka hadi Ruiru kaunti ya Kiambu, ndiyo tu ya safu moja ikilinganishwa na zile za Western bypass na Eastern bypass.

Msongamano mkubwa wa magari hushuhudiwa kwenye barabara hiyo na kusababisha kuchelewa kwa safari, gharama kubwa ya usafiri, ongezeko la uchafuzi na kupunguza uzalishaji.

Website |  + posts
Share This Article