Mihadarati yanaswa katika uwanja wa ndege wa JKIA

Tom Mathinji
1 Min Read
Mihadarati yanaswa katika uwanja wa ndege wa JKIA.

Maafisa wa upelelezi wa makosa ya jinai DCI, siku ya Jumanne walinasa mihadarati katika uwanja wa ndege wa kimataifa Jomo Kenyatta JKIA.

Kulingana na DCI, mihadarati hiyo ilikuwa ikisafirishwa kutoka Bunjumbura, Burundi hadi nchini Australia.

Kupitia ukurasa wa X, DCI ilisema mihadarati hiyo ilikuwa imefichwa ndani ya mishuma 10 na kuwekwa kwenye katoni kubwa ili kuepuka kutambuliwa.

Mihadarati hiyo iligunduliwa baada ya ukaguzi wa kina wa mizigo katika kituo cha mizigo cha DHL.

Kwa sasa mihadarati hiyo inazuiliwa huku uchunguzi ukiendelea kuwatafuta waliokuwa wakiisafirisha.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *