Serikali kufungua maabara za kidijitali kote nchini

Tom Mathinji
1 Min Read
Serikali itafungua maabara za kidijitali kote nchini.

Waziri wa habari, mawasiliano na uchumi dijitali Eliud Owalo, amesema serikali itafungua maabara ya digitali kwenye wadi zote na masoko nchini, kwa lengo la kuwapa vijana na wafanyibiashara ujuzi wa kiteknologia wa kufanya kazi na biashara za kimtandao.

Akizungumza baada ya uzinduzi wa maabara ya kidijitali katika chuo cha kiufundi cha Tinderet kwenye kaunti ya Nandi, Owalo ambaye aliandamana na katibu wake mkuu John Tanui, alisema kuwa wizara yake imezindua maabara 186 katika vyuo mbali mbali vya anuwai na kiufundi na tayari vijana 390,000 wamepata mafunzo huku 135,000 wakipata kazi ya kimtandao.

Kwa upande wake, Tanui alisema kuwa serikali inalenga kuwavutia wawekezaji hivyo itaweka mtandao katika kila taasisi ya serikali na kuwataka vijana kuchukua hatua hiyo kujinufaisha.

Kauli za wawili hao ziliungwa mkono na mjumbe wa Tinderet Julius Melly, ambaye aliwataka vijana wa eneo hilo kujiepusha na unyuaji pombe na kukumbatia maendeleo ya dijitali.

TAGGED:
Share This Article