Serikali imekariri kujitolea kukamilisha ujenzi wa miradi ya viwanja iliyokwama kote nchini na kuimarisha ukuzaji wa talanta kuanzia mashinani.
Akizungumza leo katika makao makuu ya wizara ya michezo, wakati kukabidhiana kwa mamlaka kwa katibu anayeondoka na mrithi wake, Waziri wa Michezo Salim Mvurya, amesema kuwa viwanja ni muundo msingi, muhimu katika ukuza vipaji.
“Kama serikali, tumejitolea kusuluhisha changamoto zote za miundo mbinu ya michezo nchini. Tunashirikisha wadau wote ili kuhakikisha viwanja ambavyo ujenzi wake umekwama vinaharakishwa na kukamilishwa haraka iwezekanavyo.” akasema Mvurya
Aidha, waziri amesema kuwa ujenzi unaoendelea wa akadamia 37 za michezo unalenga kuimarisha ukuzaji vipaji.
Mvurya pia ametoa onyo kali kwa mashirikisho ya michezo nchini ambayo hayajazingatia sheria za michezo zilizowekwa .
Waziri alisema haya leo aliposhuhudia ukabidhi wa mamlaka ya katibu Peter Tum anayeondoka kwa mrithi wake Elijah Mwangi.