Serikali kuangazia maslahi ya wanaoishi na ulemavu kote nchini

Martin Mwanje
1 Min Read

Serikali kupitia Hazina ya Kitaifa ya Walemavu Nchini sasa inasema kuwa imetenga kima cha shilingi zaidi ya milioni 100 mwaka huu kufadhili miradi mbalimbali ya ulemavu kote nchini.

Hii ni kulingana na afisa wa mipango wa hazina hiyo Amos Okeyo.

Akizungumza mjini Malindi kaunti ya Kilifi baada ya kuwagawa vifaa wanaoishi na ulemavu katika eneo hilo, afisa huyo alisema jumla ya waathiriwa 25 wa ulemavu wamenufaika mjini Malindi pekee.

Okeyo anasema hazina hiyo inakumbwa na changamoto za fedha huku idadi ya walemavu wanaotuma maombi ya ufadhili ikionekana kuwa juu hadi watu 10,000 kila mwaka.

Haya yanajiri huku hazina hiyo ikilenga kufadhili watu 3500 pekee kila mwaka kufuatia changamoto za kifedha.

Kwa upande wake, Naibu Kamishna wa kaunti ya Kilifi mjini Malindi Judith Mulei anasema walemavu wamekuwa wakitengwa mno eneo hilo kutokana na hali zao hivyo amesisitiza haja ya hamasa zaidi kutolewa dhidi y hatua hiyo ili kukomehsha unyanyapaa dhidi ya watu wanaoishi na ulemavu.

Afisa huyo amewataka wanaoishi na ulemavu kuripoti visa vyovyote vya udhalimu dhidi yao ili hatua za kinidhamu zichukuliwe mara moja dhidi ya wahusika.

Share This Article