Serikali itaimarisha uchumi wa baharini, asema Rais Ruto

Tom Mathinji
1 Min Read
Rais William Ruto katika mdahalo na wananchi kaunti ya Kisumu.

Rais William Ruto amesema serikali ya kitaifa itawekeza shilingi bilioni 1.5, ili kujenga vituo kumi vya uvuvi wa samaki katika ziwa Victoria.

Akizungumza leo Alhamisi katika mdahalo na wananchi kaunti ya Kisumu, kiongozi wa taifa alisema eneo la Nyanza lina fursa tele za kukuza uchumi wa eneo hilo.

Alisema serikali inajikakamua kuongeza mapato kutoka sekta ya uchumi wa baharini, hadi shilingi bilioni 100 kutoka shilingi bilioni 20 kila mwaka.

“Tumepoteza takriban watu 5,000 katika ziwa Victoria kutokana na vifaa duni. Ikiwa tutahakikisha usalama wa shughuli za uvuvi, tutawavutia watu wengi katika uvuvi,” alisema Rais Ruto.

Rais Ruto alitoa wito kwa wakenya kushirikiana na kudumisha amani, ili kulisukuma mbele gurudumu la taifa hili.

TAGGED:
Share This Article