Karitu katika Wizara ya Usalama wa Taifa Dkt. Raymond Omollo amesema serikali inajenga nyumba 47,000 za maafisa wa usalama kote nchini.
Dkt. Omollo amesema kuwa nyumba za maafisa wa usalama ni mojawapo wa nguzo muhimu katika mpango unaoendelea wa ujenzi wa nyumba za gharama nafuu.
Kulingana na Katibu huyo, nyumba hizo zitawapatia maafisa mazingira salama ya kutekeleza majukumu yao.
Aliyasema hayo wakati wa mkutano wa 14 wa kamati ndogo ya utekelezaji wa maendeleo ya kitaifa.
Mkutano huo uliwaleta Makatibu wa wizara na maafisa wakuu wa idara mbalimbali.
Serikali inatekeleza ujenzi wa nyumba za gharama nafuu kote nchini, kwa lengo la kuboresha maisha ya wakenya.