Serikali imetangaza kesho Jumatano kuwa siku kuu ya Id ul fitr.
Waziri wa usalama wa taifa, Prof. Kithure Kindiki alitoa tangazo hilo leo Jumanne asubuhi, kupitia arifa kwenye gazeti rasmi la serikali.
“….Kulinagana na mamlaka niliyopewa kupitia sehemu ya 2 (1) ya sheria za siku kuu, Waziri wa usalama wa taifa ametangaza Jumatano Aprili 10 2023, kuwa siku kuu ya kuadhimisha Idd ul-Fitr,”- alisema Waziri Kindiki kupitia gazeti rasmi la serikali.
Siku kuu ya Eid ul fitri huadhimisha kukamilika kwa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa waumini wa dini ya Kiislamu.
Waislamu walianza mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhan, tarehe 11 mwezi Machi.