Serah Teshna atangaza uwepo wa mwanao wa pili

Marion Bosire
1 Min Read

Mwigizaji wa Kenya Serah Teshna ametangaza kwamba yeye na mcheza soka Victor Wanyama walibarikiwa na mwanao wa pili yapata miezi mitano iliyopita.

Alichapisha picha ya wanyama na mtoto huyo kwenye Instagram na kuandika, “Miezi mitano ambayo imepita imekuwa ya upendo mwingi, furaha, vicheko, matatizo kiasi na kukosa kulala usiku.”

Teshna aliendelea kusema kwamba wanapenda hali ilivyo na kwamba mtoto huyo kwa jina Gigi amekamilisha muunda wao wa mraba ambao alisema ni kamili.

“Kukutizama ukihusiana na nduguyo mkubwa ni kila kitu tulichoomba. Anasubiri sana utembee ili mcheze.” Aliandika mwigizaji huyo huku akimalizia kummiminia mtoto huyo mapenzi tele.

Serah na wanyama wamekuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi kwa muda mrefu na mwaka jana Teshna alifichua kwamba wako kwenye ndoa.

Mwigizaji huyo aliamua kuacha kazi yake humu nchini na kuhamia Canada ambako Wanyama anachezea.

Alisema awali kwamba kazi yake ya uigizaji ilikuwa inachukua muda wake mwingi kiasi kwamba hakuwa anaweza kukaa na mwanawe wa kwanza inavyostahili.

Share This Article