Simba wa milima ya Teranga ,Senegal,Pharoes ya Misri na swara wa Palancas kutoka Angola, zimejikatia tiketi kwa makala ya 35 ya fainali za kombe la bara Afrika AFCON, mwaka 2025 nchini Morocco.
Senegal ilihitaji bao la dakika za mwisho lake Sadio Mane ili kuwashinda Malawi ugenini katika kundi L na kufuzu wakiwa na alama 10 sawa na Burkina Faso.
Chui wa Congo nao walifuzu kwa fainali za Morocco kufuatia ushindi wa magoli mawili kwa bila ugenini Dares Salaam dhidi ya Tanzania,wakiongoza kundi H kwa pointi 12.
Misri ambao wanajivunia kutwaa mataji mengi zaidi ya AFCON yakiwa 7, nao walifunga safari ya Morocco, kufuatia ushindi wa goli moja kwa nunge ugenini dhidi ya Mauritania kundini C.
Morocco almaarufu Atlas Lions ambao tayari wamefuzu kama waandalizi pia walisajili ushindi wa nne mtawalia wakiongoza kundi B kwa pointi 12.
Mataifa manane yamefuzu kwa kipute hicho yakiwa ni;Algeria,Misri,Angola,Cameroon,Senegal,DR Congo,Burkina Faso na wenyeji Morocco.
Fainali za 35 za AFCON zitaandaliwa katika baina ya Disemba 21 mwaka 2025 na Januari 18 mwaka 2026 katika viwanja sita vilivyo katika miji sita ya ;Rabat,Casablanca,Agadir,Fez,Marrakesh na Tangier.