Senegal yamtimua kocha mkuu Pape Thiaw na wasaidizi wake wote

Thiaw, aliye na umri wa miaka 45, anakumbukwa sana kwa kuwaongoza wachezaji kuondoka uwanjani katika fainali ya kombe la AFCON mwezi Januari mwaka huu kupinga penalti iliyopewa wenyeji Morocco.

Dismas Otuke
1 Min Read

Shirikisho la Soka nchini Senegal limetangaza kumtimua kocha mkuu wa Teranga Lions Pape Thiaw na wasaidizi wake wote.

Hii ni kufuatia matokaeo mabovu ambapo timu hiyo ilibanduliwa katika hatua ya 32 ya Kombe la Dunia na Ubelgiji.

Aidha, Senegal ilishinda mechi moja pekee ya kundi lao mabao 5-0 dhidi ya Iraq, ndiposa ikafuzu kwa hatua ya 32 bora.

Kocha huyo anatimuliwa baada ya kuongeza mkataba wa kuifunza Teranga Lions kabla ya kuanza kwa Kombe la Dunia mwaka huu.

Thiaw, aliye na umri wa miaka 45, anakumbukwa sana kwa kuwaongoza wachezaji kuondoka uwanjani katika fainali ya kombe la AFCON mwezi Januari mwaka huu kupinga penalti iliyopewa wenyeji Morocco.

Share This Article