Sehemu kadhaa za nchi zakosa nguvu za umeme

Tom Mathinji
1 Min Read

Sehemu kadhaa za hapa nchini zimeghubikwa na giza totoro, kutokana na  kupotea kwa nguvu za umeme, Ijumaa usiku 

Kampuni ya usambazaji nguvu za umeme KPLC,  imethibitisha kuwa umeme umepotea katika sehemu zote za nchi isipokuwa maeneo ya North Rift na sehemu kadhaa za Magharibi mwa nchi.

“Tumepoteza umeme katika sehemu kadhaa za nchi isipokuwa sehemu kadhaa za North Rift na Magharibi mwa nchi,”  ilisema taarifa ya KPLC Kupitia mtandao wa X Ijumaa usiku.

“Tunasikitikia hali hiyo na tunawahimiza wateja wetu kuwa watulivu tunapojizatiti kurejesha hali ya kawaida haraka iwezekanavyo,” iliongeza taarifa hiyo.

Kupitia mitandao ya kijamii, wakenya kutoka pembe tofauti za nchi  wamelalamikia ukosefu wa nguvu za umeme.

Hii si mara ya kwanza kwa taifa hili kukumbwa na ukosefu wa nguvu za umeme ambao unaathiri sehemu kubwa ya nchi.

TAGGED:
Share This Article