Ubalozi wa Saudi Arabia nchini Lebanon umewataka raia wake kuhama kutokana na mapigano yanayoendelea baina ya makundi hasimu ya Wapalestina walio nchini Lebanon.</strong
Lebanon imeonya kuwa huenda majeshi yakaingia kati endapo mapigano kati ya pande hasimu yataendelea nchini Palestine.
Hata hivyo Saud Arabia haikutoa taarifa kamili kuhusu maeneo ambayo raia wake wanapaswa kuepuka nchini Lebanon.
Mapigano hayo yameingia siku ya tatu mtawalia .
Kuwait pia imetoa tahadhari kwa raia wakke dhidi ya kuzuru Lebanon huku ikiwataka raia wanaoishi humo kuwa macho.
Watu 13 wameua tangu Julai 29 na wengine zaidi ya 60 kujeruhiwa katika mapigano hayo kati ya kundi la Fatah na kundi jingine asi.