Mwigizaji wa Nigeria Sarah Martin amemwomba msamaha May Yul Edochie ambaye ndoa yake na mwigizaji Yul Edochie iligonga mwamba.
May alitengana na Yul baada yake kuoa mwigizaji Judy Austin na Sarah Martins ni mmoja wa watu ambao walimdhalilisha mitandaoni.
Baada ya video za kongamano fulani la wanawake kusambaa mitandaoni ambapo May alikuwa mmoja wa waliohutubia kongamano hilo kusambaa, wengi wamebadili mawazo kumhusu.
Alisimulia kuhusu ndoa yake ilivyoingiliwa kiasi cha kuwaliza waliohudhuria kongamano hilo.
Martins ametoa ombi hilo la msamaha kupitia mitandao ya kijamii ambapo alichapisha mojawapo ya video za hotuba ya May kwenye kongamano hilo.
“Dada acha huyo mwanaume ateseke na yule alidhania ni bora zaidi yako.” aliandika sarah huku akikiri kwamba ametambua May ndiye alikuwa anasababisha Yul apate ukuu.
Sarah anamshauri May sasa aangazie maisha yake binafsi bila kujali huku akimtaka kuwa mwanamke wa nguvu.
“Nitajuta milele kwa jinsi niliwakubalia wanitumie dhidi yako. Tafadhali nisamehe.” alimalizia mwigizaji huyo.
May na Yul wametangana tu ila hawajatalikiana kulingana na shangazi ya Yul ambaye pia ni mwigizaji Rita Edochie. Uvumi ulisambazwa mitandaoni awali kwamba May alikuwa amekwenda mahakamani kuanzisha mipango ya talaka.