Sakaja azindua afisi mpya za kaunti kuboresha huduma

Dismas Otuke
1 Min Read

Gavana wa kaunti ya Nairobi Johnson Sakaja jana Alhamisi alizindua afisi mpya za kaunti hiyo katika jitihada zinazolenga kuboresha utoaji huduma kwa umma.

Afisi hiyo ijulikanayo kama City Hall Annex ilijengwa kwa gharama ya shilingi milioni 100.

Gavana Sakaja alisema kuwa wateja watapata huduma zote za jiji katika afisi hiyo ikiwemo leseni kwa njia rahisi na ya kisasa.

“Kwa wale ambao mmetembelea City Hall Annex, mtafurahi kuona ukarabati ambao tu ndio umemalizwa na Kituo Kipya cha Utoaji Huduma kwa Wateja ambacho tumezindua leo. Kimeboreshwa zaidi, tuna timu zetu ambazo zimepewa mafunzo zikisubiri kuwahudumia,” alisema Sakaja.

 

Jengo zilipo ofisi hizo halijakarabatiwa kwa miongo kadhaa iliyopita.

Share This Article