Sakaja aondoa marufuku ya ujenzi

Kevin Karunjira
2 Min Read

Gavana wa kaunti ya Nairobi Johnson Sakaja, ameondoa marufuku ya kukagua ramani za ujenzi jijini. Marufuku hayo yaliwekwa kutokana na mafuriko ya hivi maajuzi yaliyo waua watu wengi, kuharibu mali na kuchelewesha shuguli nyingi.

Vile vile, ameondoa marufuku ya vibali vya ukarabati wa majumba yaliyoathiriwa na mafuriko.Ada za ukarabati huo pia zimeondolewa.

Kufuatia uamuzi huo, serikali ya kaunti imeadaa mkutano na wawakilishi wa washika dau wa kaunti hiyo. mkutano huo wa tarehe 12 Juni, utabuni mwongozo wa zoezi la kutathmini hali halisi ya ujenzi jijini na kutoa mapendekezo ya siku za usoni. Shughuli hiyo itachukua siku 60 na maafikio kupewa gavana kwa utekelezwaji.

Zaidi ya hayo, Sakaja amebuni kamati ya kiufundi ya jijini-UPTC na kuwaalika wawakilishi kutoka bodi za waratibu wa miji, wanamazingira, wahandisi na wasanifu mijengo.lengo la UPTC ni kutathmini na kupendekeza utoaji wa vibali vya ujenzi.

Hatua hii ya Gavana kuondoa marufuku hayo, inajiri wakati kesi iliyowasilishwa kortini kupinga maamuzi yake itasikilizwa na kuamuliwa hapo kesho.

Katika kesi hiyo, mlalamishi Victor Odhiambo alidai kuwa uamuzi wa Sakaja wa kupiga marufuku shughuli za ujenzi ulikuwa kinyume cha katiba na alikiuka haki za kiutawala za kifungu cha 4(3). Pia, alijitwika jukumu la kamati ya utendaji wa kaunti hiyo- CEC inayoongozwa na Stephen Mwangi.

Share This Article