Msanii wa muziki wa asili ya Rwanda Niyibikora Safi maarufu kama Safi Madiba, alirejea jijini Kigali nchini Rwanda baada ya miaka minne nchini Canada.
Aliandaa tamasha la kurejea nyumbani usiku wa jana Jumamosi Disemba 7, 2024 katika eneo la burudani la Green Lounge huko Kicukiro, pamoja na Phil Peter, Muyango Claudine na DJ Brianne.
Safi alifurahia kurejea nyumbani na kuungana tena na watu wa nyumbani huku akiwapa fursa ya kufurahikia albamu yake iitwayo “Back to Life” aliyotoa mapema mwaka huu.
Tamasha hilo ndilo la kwanza la Madiba jijini Kigali tangu alipotoka kwenye kundi la wanamuziki la Urban Boys na kuanza kuimba peke yake.
Tangu alipohamia canada, Madiba amerekodi nyimbo kadhaa na kutumbuiza kimataifa nchini canada, Marekani na hata Ufaransa.
Katika albamu “Back to Life” Safi ameshirikiana na wasanii kama Meddy, Harmonize na Rayvanny.
Nyimbo za albamu hiyo kama vile ‘Got It’, ‘Nisamehe’ na ‘One a Million’ zimepokelewa vyema na wasikilizaji huku akirejelea albamu hiyo kama onyesho la jinsi alivyokua katika muziki.
Safi aliondoka kwenye Urban Boys mwaka 2018 kutokana na tofauti fulani lakini anatambua kwamba kundi hilo ni muhimu kwatika msingi wake kwenye muziki.