Safaricom yakana kutoa taarifa za wateja

Martin Mwanje
1 Min Read
Peter Ndegwa, Afisa Mtendaji wa Safaricom

Kampuni ya Safaricom imekanusha madai kuwa imekuwa mbioni kutoa taarifa za wateja kwa taasisi za serikali. 

Katika taarifa hiyo, kampuni hiyo inasema inaweza ikatoa taarifa kwa taasisi yote ile ikiwa tu kuna agizo la mahakama.

“Tunaheshimu ufaragha wa wateja wetu na kuzingatia vikali sheria za ulinzi wa data za nchi yetu. Kutokana na hilo, hatupatiani taarifa zozote za mteja isipokuwa tukitakiwa kufanya hivyo na agizo la mahakama,” ilisema Safaricom katika taarifa.

“Kuhusiana na suala la sasa linalojadiliwa, tunathibitisha kuwa hatujapokea agizo lolote la mahakama linalotutaka kutoa taarifa za wateja kwa taasisi yoyote ya serikali.”

Taarifa hiyo inafuatia madai kuwa kampuni za mawasiliano nchini zinatoa taarifa za wateja kwa vyombo vya usalama zinazosaidia katika utekaji nyara unaoshuhudiwa nchini.

Utekaji nyara huo umedaiwa kutekelezwa na maafisa wa usalama.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *