Safaricom yadhamini timu ya Kenya ya Olimpiki kwa kima cha shilingi milioni 30

Dismas Otuke
1 Min Read

Kampuni ya kutoa huduma za mawasiliano ya Safaricom,kupitia kwa wakfu wa M-PESA imetoa ufadhili wa shilingi milioni 30 kwa timu ya Kenya, itakayoshiriki makala ya 31 ya Michezo ya Olimpiki yatakayoandaliwa jijini Paris Ufaransa kati ya Julai 26 na Agosti 11 mwaka huu.

Kima hicho cha ufadhili kinajumuisha muda wa maongezi na data ,bima kwa wanariadha ,mafunzo ya uwekezaji na kutoa mavazi kwa wanariadha watakapokuwa kambini.

Kwenye mkataba huo Safaricom wako huru kutoa majina yatakayotumiwa kwa kambi za timu ya Kenya,kuendesha shindano la uchoraji na ubunifu wa kibonzo rasmi cha timu ya Kenya uhuru wa kutoa mafunzo ya kifedha na uwekezaji kwa timu ya Kenya itakapokuwa kambini.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *